Numbers 23:7-11

7 aNdipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki amenileta kutoka Aramu,
mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki.
Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo;
njoo unishutumie Israeli.’

8 bNitawezaje kuwalaani,
hao ambao Mungu hajawalaani?
Nitawezaje kuwashutumu
hao ambao Bwana hakuwashutumu?

9 cKutoka vilele vya miamba ninawaona,
kutoka mahali palipoinuka ninawatazama.
Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao,
nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa.

10 dNi nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo,
au kuhesabu robo ya Israeli?
Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki,
na mwisho wangu na uwe kama wao!”

11Balaki akamwambia Balaamu, “Ni nini ulichonitendea? Nimekuleta ulaani adui zangu, lakini wewe badala yake umewabariki!”

Copyright information for SwhKC